Kutokuelewa Sharia kwamkandamiza mwanamke – Dr Ziddi.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dr Issa Haji Ziddi amesema kutokuelewa sharia kwa wanawake na wanaume kwa kufuata zaidi mila na utamaduni ndiyo sababu iliyopelekea mwanamke kufanywa dhalili na mnyonge.

Hayo ameyasema alipokuwa akiwasilisha mada juu ya nafasi ya mwanamke wa kiislam katika semina ya siku mbili ya wanawake wa kiislam iliyofanyika katika ukumbi wa bwawani mjini Zanzibar.

Amesema Uislam haujamlazimisha mwanamke au mwanamme kuwa ni mhudumu au mfanyakazi wa nyumbani  bali inatokana na wahusika wenyewe kutofuata mafunzo ya dini kwa kukusudia kuwanyanyasa wanawake kwa kufasiri mafunzo ya dini katika kidume dume na kwa kupenya kuwa mwanamme lazima awe juu.

Dr Ziddi amefahamisha kuwa hali hiyo imepelekea mwanamke kuangaliwa kuwa dhalili, tegemezi na mnyonge ambae si mkamilifu wa dunia wala dini katika jamii.

“Na ukweli mfumo huu ni wa hatari sana na huenda ndio unaochangia mporomoko wa maadili unaotajwa kila siku na watu mbali mbali katika jamii yetu,” alisema Dr Ziddi.

Hata hivyo amesema mwanamke halazimishwi na sheria na haulizwi kwa nini hakumhudumia mume au kama hakufanya kazi za ndani ya nyumba bali hufanya kwa mapenzi yake na kwa kujitolea ambapo alisisitiza kuwa hupata malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu (S.W).

“Jambo baya ni kule kujitolea huko ichukuliwe kuwa ni wajibu kama ilivyo sasa. Kama atajitolea kwa kazi hizo basi ichukuliwe kuwa ni njia za kuonesha huruma na utu wake kwa wale walio karibu zaidi nay eye mume na watoto,” alifahamisha.

Akitoa mada juu ya mwanamke wa kiislam katika kupambana na Ukimwi katibu wa Mufti Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga amesema silaha kubwa itakayowaokoa watu ni kukubali kubadili tabia, amesema Afisi ya Mufti Mkuu Zanzibar inapinga vikali propaganda inayoenezwa ulimwenguni juu ya matumizi ya Kondom na msemo wa ngono salama.

Aidha Sheikh Soraga amewataka waislam kuachana na tabia ya kuwanyooshea vidole waathirika kwa nia ya kuwakebehi na kuwahimiza kuwafariji waathirioka hao pamoja na kuwasitiri ili waweze kufanikiwa katika maisha yao.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s