Chuo cha Kiislam Zanzibar chatoa wahitimu

Mke wa Rais wa Zanzibar mama Shadya Karume amewataka wahitimu  wa Chuo cha Kiislam kurejesha maadili ya chuo katika elimu ya Kiislam kwa vile kimeshatoa wataalamu wengi ambao hivi sasa wanategemewa na Serikali.

Amesema kufanya hivyo kutasaidia kurudisha maadili mema yanayoendelea kuporomoka katika jamii.

Mama Shadya  ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mahafali ya nane ya Chuo cha Kiislamu kilichopo Mazizini nje kidogo na mji wa Zanzibar.

Akijibu risala ya wahitimu hao wa mafunzo ya ualimu juu ya matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo amesema Serikali inaendelea kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayoikabili sekta ya elimu ili kuwa mazingira bora  ya utoaji wa taaluma kwa vijana mbapo aliahidi kuchgangia shilingi Laki tano kwa kamati ya Daawa inayoendeshwa chuoni hapo.

Amesema malengo ya taasisi za elimu na vyuo ni kuwaandaa vijana kuwa na ufahamu jambo ambalo litafikiwa ikiwa hakutakuwa na vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ya sekta hiyo.

Mama Shadya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAYEDESA amewataka wahitimu hao kueneza elimu juu ya athari ya dawa za kulevya, ugonjwa wa ukimwi pamoja na maadili mema katika mazingira wanayoishi.

Akizungumza katika mahafali hayo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Haroun Ali Suleiman amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka ujao wa fedha watatenga fedha maalum ya kujenga chuo kipya cha kisasa kinachoendana na hadhi ya majengo ya wizara ya elimu.

Amesema eneo la chuo hicho ni vyema kuboreshwa kwa kujengwa chuo kipya ili jengo liweze kuendana na hadhi ya elimu inayotolewa chuoni hapo na hatimae chuo hicho kuweza kufikia hadhi ya kuwa Chuo Kikuu.

Katika risala yao wahitimu hao wamesema wanakabiliwa na uhaba wa vifaa vya maabara na hivyo kushindwa kufanya majaribio ya vitendo katika masomo ya sayansi.

Wahitimu wapatao mia mbili na hamsini wa ngazi ya diploma katika fani tofauti wamekabidhiwa vyeti na zawadi mbali mbali.

Mhafali hayo yamefanyika kwa mashirikiano ya Chuo Cha Kiislam kwa ufadhili Jumuiya ya Muzdalifah

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s