Madrasa zawawezesha wanafunzi kufaulu katika mitihani yao

Wanafunzi wanaosoma madrasa za Kiislamu wana ufahamu mzuri kiakili   katika kujitafutia elimu.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Muzdalifah Islamic  Charitable Organization Sheikh Abdallah Hadhar katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wanawake wa AL- Madrasat Aminna Islamiya iliyopo Kilimani.

Amesema katika utafiti uliofanywa imebainika kuwa wanafunzi wanao soma  Madrasa wanashika nafasi za mwanzo maskulini na kwamba madrasa ni miundo mbinu ya waislamu.

Hivyo amewataka wanafunzi hao kuzidisha juhudi katika masomo yao kwani wankila sababu ya kufanya vizuri.

Sheikh Abdallah amewahimiza wanafunzi hao kusoma zaidi masomo ya dini na dunia ili waweze kuwa viongozi wazuri baadae kwani mtu anaejua dini anakuwa kiongozi mzuri.

Amesema Ili kwenda sambamba ni lazima wasome masomo ya dunia kama sayansi na Art kwani ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa kusoma na kuwataka kufahamu kuwa wanaposoma wanausaidia Uislamu sana na wataweza kujiajiri wenyewe hapo baadae.

Akitoa shukrani zake kwa Jumuiya ya Muzdalifah Ustadh Adam H. Makusanya amewataka wanafunzi hao kuwa tayari kupambana na mbinu za Makafiri.

Amesema Uislamu umempa hadhi mwanamke kwa kumkomboa kutoka katika udhalimu na kuwataka wajipange zaidi kwa kuwa waislamu wanatakiwa kuwa mbele zaidi katika Elimu.

Ustadh Farouk Hamad ambaye ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Muzdalifah amesema Jumuiya ya Muzdalifah inatarajia kujenga Hostel (dakhalia) kwa lengo la kuwalea katika mazingira mazuri ya dini. Pia na kuwatafutia nafasi za masomo ndani nje na ya nchi, ambapo alisema ukimsomesha mwanamke mmoja ni sawa na kusosomesha watu kumi.

Hivyo amesema ni vyema kuwasomesha watoto wa kike na kuwalea katika maadili mazuri ili kupata walezi wazuri wa familia pamoja na viongozi wazuri ha[po baadae.

 Jumuiya ya Muzdalifah imetoa msaada wa vitambaa wenye gharama ya shilingi laki tano za kitanzania kwa Almadrasat Aaminat Islamiyah yenye jumla ya wanafunzi 120.

Advertisements

2 Replies to “Madrasa zawawezesha wanafunzi kufaulu katika mitihani yao”

 1. Salaam, nashukuru sana kuona kuwa Waislamu wa Zanzibar hasa wanawake wapo mstari wa usoni kufanya Da’awa kwa njia za kileo ikiwemo hii ya kutumia teknolojia ya habari ili kufikisha ujumbe kwa watu walio wengi zaidi.
  Allah azidi kuwapa nguvu wasimamizi wa mradi huu. Dua yangu kwa Mwenye enzi Mungu ni kuwa awajaalie waendeshaji wa mradi huu wawe na subra kubwa kwa sababu jambo jema kama hili halitakwenda hivi hivi tu bila ya kupata mitihani. Jambo la msingi ni kuwa na hekima, maarifa na kupima matukio na hali halisi kwa mizani ya uelewa na lengo la kuundeleza mradi huu milele. Miradi mingi mizuri huanzishwa lakini hukatika njiani.
  Asanteni ndugu zangu na inshaAllah mufanikiwe kutuelimisha.
  Ziddy

  1. Asalam Aleykum,
   Kwanza namshukuru Allah Subhanahu Wataala kwa kuniwezesha kuanzisha Blog hii.
   Pili nashkuru sana kupata michango na changamoto nzuri kutoka kwako Dr Ziddi namuomba Allah akuzidishie kila la kheri wewe pamoja na Waislam wote na aweze kutupa nguvu Waislam ili tuweze kufanikiwa Duniani na Akhera na tuingie katika Jannah.
   JAZAAKALLAHU L KHAIR

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s