Uamsho kufanya Mkutano Mkuu wa Wanawake.

Jumuia ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar  inatarajia kufanya Mkutano mkuu wa wanawake utakaochagua viongozi watakaofanyakazi zinazolingana na mfumo wa Jumuiya yenyewe ili kuhakikisha kuwa Jumuiya hiyo inafanya kazi kwa usawa.

Hayo yamesemwa na viongozi wa Jumuiya hiyo katika Mkutano Mkuu uliofayika Juni 27 katika ukumbi wa Jamat Khan mjini Zanzibar.

Katika mkutano huo Jumuiya hiyo imepata viongozi wapya watakaoiongoza  kwa kipindi cha miaka mitatu.

Waliochaguliwa katika mkutano mkuu uliofayika Juni 27 katika ukumbi wa Jamat Khan mjini Zanzibar ni Amiri mkuu Sheikh Haji Khamis Haji,  Katibu mkuu ni Ustadh Abdallah Said Ali (maarufu Abdallah madawa) na Ustadh Azan Khalid Hamdan amechaguliwa kuwa Naibu Katibu mkuu. 

Wengine waliochaguliwa ni wajumbe watano wa Bodi ya wadhamini itakayoongozwa na Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Ustadh Abdulrahiim Salim ni Maalim Talib Mahadhi, Najim Abdallah Najim, Ali Muhammed  Mselllem Aliy na Farid Aliy Ahmed.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo ulijadili taarifa za utekelezaji wa kazi kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kuweka mikakati kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kwa kupitia kamati mbali mbali za usimamizi za utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya hiyo.

Kamati hizo ni pamoja na Kamati ya Mihadhara, Maafa, Kupambana na vileo(ulevi) na Kamati ya uchumi na fedha.

Mkutano wa tatu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar ulihudhuriwa na waislam mbali mbali pamoja na kufanyika kwa uzinduzi wa Weblog ya Jumuiya  ambayo inajulikana kwa anuani ya www.uamshozanzibar.wordpress.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s