Vyombo vya Habari vina mchango mkubwa katika Malezi -Wanawake UKUEM

Vyombo vya habari vinatoa mchango mkubwa katika malezi ikiwa vitatumiwa ipasavyo kwa kuwa huchukua nafasi ya kitabu kutokana na mafunzo yanayotolewa.

Hayo ameyasema Amirat wa kitengo cha Habari cha wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi, Elimu na Maendeleo (UKUEM) Ukhty Talhiya Masoud Salum alipokuwa akizungumza katika kikao cha wanawake wa Kiislam kilichofanyika katika Ukumbi wa Al- Madrasat Falaah Kijangwani Zanzibar.

Akitoa mada juu ya malezi ya Kiislam kwa vyombo vya habari amesema vyombo vya habari vya Kiislam kama radio za Kiislam kama Imaan Fm zimekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha jamii kimaadili na kwamba jamii ya Kiislam imekuwa inapata mambo mengi sana kielimu, kidini na kidunia.

Amefahamisha kuwa ikiwa vyombo hivyo vitajiandaa katika kukuza maadili jamii itaweza kuelekea katika maadili mazuri ambapo amesema endapo itakuwa kinyume na hivyo zitaharibu maadili baada ya kutengeneza.

“Na kinyume chake tuangalie Bomba fm na Chuchu fm hizi ni radio ambazo zinaharibu maadili ya Kiislam. ….Kama vyombo vya Serikali au binafsi vijue kuwa vina jukumu kubwa katika kukuza maadili ya Kiislam. Na hasa TV maana ndio mtoto au watu waanjionea hali halisi ya maharibiko au maelekezo,” alisema Ukhty Talhiya.

Aidha amewataka wanawake wa Kiislam kujidhatiti kwa katika kushirikiana na wenaoshughulikia malezi pamoja na kuwa tayari kufuata mafundisho ya Qu-ran na Sunna kivitendo pamoja na kuzingatia kuwa wao ni wachunga na wataulizwa kwa walichokichunga.

Hivyo amewataka wanawake wa Kiislam kuvitumia vyombo vya habari vya Kiislam ili kuweza kupata elimu sahihi ya maadili ya Kiislam katika maisha yao ya kila siku na kuachana va vyombo vinavyochangia kuharibu maadili pamoja na kujenga utamaduni wa kusoma Magazeti ya Kiislam.

Kikao hicho kimeandaliwa na wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi, Elimu na Maendeleo (UKUEM) chini ya Al- Madrasat Falaah Kijangwani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s