Ukuem waikaribisha Ramadhan kwa onesho maalum.

Wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi Elimu na Maendeleo wanatarajia kufanya onesho maalum la kuukaribisha Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani.

Onesho hilo linalotarajiwa kuhudhuriwa na wanawake mbali mbali litafanyika katika ukumbi wa Jamat Khan Vuga mjini hapa kuanzia Ramadhan mosi hadi tano na litaambatana na mihadhara itakayotolewa na wahadhiri mbali mbali.

Akizungumza na Blog ya MWANAMKE WA KIISLAM katika Skuli ya Haile Sealassie Mjumbe kutoka katika kamati ya Habari na Mawasiliano wa jumuiya hiyo Ukhty Asha Juma Suleiman amesema onesho hilo litaonesha mambo wanayotakiwa  waislam wayafanye   katika kipindi cha Mwenzi mtukufu wa Ramadhan.

 “Tumeandaa onesho la kuukaribisha mwenzi mtukufu wa Ramadhani kwa ibada mbali mbali wanawake wasijishighulishe zaidi na mapishi, Ramadhani imefika lakini watu wanashughulika zaidi na mapishi na wanakuwa wavivu kufanya ibada pamoja na kujishughulisha kucheza karata pamoja na laghawi na kufanya muda mwingi upotee kwa upumbavu,” alisema.

Amesema onesho hilo lina lengo la kuelimisha jamii ya Kiislam hasa wanawake kujipangilia vizuri katika shughuli zao mbali mbali tangu asubuhi hadi usiku na kuwataka kuachana na mambo yasiyofaa kama kucheza karata kamari na mengineyo yasiyotakiwa na kuwahimiza kukithirisha ibada mbali mbali kama kusali sala za Taraweih, Dhuha, Witri pamoja na Adhkaar.

Onesho hilo linatarajiwa kuchezwa na wanawake na litaoneshwa kwa wanawake watupu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s