Waislam watakiwa kujipinda katika ibada katika mwenzi mtukufu wa Ramadhaan

Wanawake wa Kiislam wametakiwa kuacha kufikiria namna gani wataandaa futari pamoja na siku kuu ya Eid El Fitr na badala yake kufikiria namna gani watashiriki kufanya ibada ili kuweza kufikia lengo la ucha Mungu.

Wito huo umetolewa na Ustadh Ali Masoud kutoka Masjid Sunna Kikwajuni alipokuwa akizungumza na wanawake wa Kiislam katika mhadhara wa kuukaribisha mwenzi mtukufu wa Ramadhaan iliofanyika August 16 katika ukumbi wa Shantimba Mombasa nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Amesema mara nyingi watu wamekuwa na tabia ya kuandaa vyakula vya kila aina pamoja na michezo mbali mbali katika mwenzi mtukufu wa ramadhani jambo ambalo ni kinyume na mafundisho ya kitabu kitukufu cha Qur-an pamoja na Sunna za Mtume Muhammad  Swalla Lllahu alayhi Wasallam.

Amefahamisha kuwa lengo la saumu ni kumtengeneza mja kuwa na vitendo pamoja na tabia njema hivyo ni vyema waumini kuitumia neema hiyo kama ilivyokusudiwa.

Amewataka waumini wa dini ya Kiislam kuhakikisha kuwa wanapata uchamungu na kuwa wanyenyekevu na kuleta athari ya kuwa wachamungu pindi itakapomalizika ramadhan kwani baadhi ya watu wamekuwa wakirudia matendo mabaya.

 Amehimiza haja ya waislam kujua thamani na utukufu wa dini yao yaliyoletwa na mwenyezi mungu na kuazimia kuwa waja wema katika mienzi yote na si kwa ramadhani pekee.

Aidha amekemea tabia ya baadhi ya watu kunasibisha maovu ya Vunja Jungu na mwenzi mtukufu wa Ramadhaan na kusema kuwa tabia hiyo ni kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislam.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s