Kufarikiana kwa Waislam ni kupoteza malengo ya Ibada- Ustadh Kassim Maabad

Kutopatikana kwa taathira ya ibada za Sala na Funga kwa Waislam Zanzibar kunatokana na kufarikiana kwa watu wake.

Hayo ameyasema Ustadh Kassim Maabad alipokuwa akizungumza na wanawake wa Kiislam katika mhadhara maalum wa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhan huko katika ukumbi wa Jamat Khan Vuga mjini hapa.

Amesema hali hiyo imepelekea kuharibika na kupotea kwa maadili ya Kiislam ambapo wazazi wamekuwa wanawalea watoto wao kinyume na ilivyoamrishwa katika dini na kusababisha hali ya Ramadhaan Zanzibar kuwa ngumu.

“Ili mgeni ajione yupo nyumbani tunatakiwa tujiandae katika mazingira mazuri ya Ucha Mungu, lakini leo mazingira yameharibika tuna hofu huu Ucha Mungu kama kweli tutaufikia sisi, tunahudhuria katika madrasa, misikitini lakini bado hatujabadilika,” alisema

Amefahamisha kuwa ili lengo la Ucha Mungu lipatikane ni lazima waumini wajihifadhi kwa kuacha makatazo na kufuata maamrisho ya Qur-an na Sunna pamoja na kuzihifadhi nafsi kwa kutosema mambo yanayoharibu amali zao.

Amewahimiza wanawake kuzitengeneza nyumba zao kwa kufanya jitihada ya kuwalea watoto wao katika maadili mema ya Kiislam ili kuwaandalia mwisho mwema Duniani na Akhera na kwamba wao ni chuo kwa kuwa muda mwingi wanawashughulikia watoto.

Mhadhara huo umeandaliwa na wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam, Uchumi, Elimu na Maendeleo UKUEM chini ya Al Madrasat Falaah Kijangwani Zanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s