Waislam wahimizwa kusoma Qur-an

Waislam wametakiwa kusoma Qur-an kwa kuzingatia hukmu zake ili kuepukana na matatizo mbali mbali katika jamii.

Wito huo umetolewa na Ukhty Hafsa Muhammad Ali katika mhadhara ulioandaliwa na wanawake wa Jumuiya wa Umoja wa Kiislam, Uchumi, Elimu na Maendeleo (UKUEM) katika ukumbi wa skuli ya maandalizi ya saateni.

Amesema endapo muislam ataitumia vizuri qur-an kwa kuisoma kama inavyotakiwa katika kuzingatia hukmu zake itamuezesha mtu kufanya vizuri katika ibada ya sala na kuondokana na matatizo mbali mbali.

Ukhty Hafsa amefahamisha kuwa wanawake wana muda mwingi wa kukaa majumbani hivyo ni vyema kwa wanawake kuutumia muda mwingi katika kuisoma Qur-an ili kuwa na maadili mema katika jamii kwani ndio mfumo wa maisha ya binaadamu.

Aidha amesema endapo mtu ataisoma qur-an bila ya kuzingatia hukmu zake atakuwa anakwenda kinyume na mazingatio ya dini na atapata laana kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s