Matajiri watakiwa kudhamini Sherehe za Kiislam

Wafanyabiashara na matajiri mbalimbali visiwani Zanzibar wametakiwa kujitokeza kwa wingi kudhamini Siku kuu za Kiislam kwa kuhakikisha wanavidhibiti viwanja vinavyosheherekewa Eid kwa kufanya sherehe hizo kwa mujibu wa taratibu za Kiislam.

Ushauri huo umetolewa na Ukhty Zakia Khamis Muhammed katika alipokuwa akijadili namna ya kuukabili mporomoko wa maadili visiwani humu katika Mhadhara wa Wanawake wa Kiislam uliofanyika katika ukumbi wa Sunni Manzil Vikokotoni mjini hapa.

Amesema ili matatizo matatizo mbali mbali yakiwemo mmomonyoko wa maadili yaondoke Zanzibar ni vyema kujitokeza kwa wadhamini na kuvidhibiti viwanja hivyo ili watoto waislam waweze kuwa katika mazingira yanayoridhiwa na Mwenyezi Mungu na Mtume (S.A.W).

Amefahamisha kuwa jukumu la kuhakikisha kuwa waislam wanaishi katika misingi ya dini yao si la mtu binafsi bali ni la kila muislam na kwamba kila mmoja atahusika katika kujibu maswali kutokana na kutowajibika au kuwajibika kwake katika jamii anayoishi.

“Kama hawa matajiri wangekubaliana hivi viwanya vya Mnazi mmoja vikawa vimedhibitiwa na waislam tukawa tunacheza michezo ya Kiislam, wanawake wakawa wamewekwa sehemu zao na wanaume sehemu zao, hao wanaopenda dunia wakawa wanakaa uchi Watajua wenyewe sehemu za kwenda kwa sababu hizo sehemu ambazo wanategemea tumeshazidhibiti sisi wenyewe waislam tayari,” alisema.

Amesema matajiri wamekuwa hawafanyi vizuri katika ibada zao kwa kuwa wanashindwa kujitokeza katika kuihami dini ya Mwenyezi Mungu kutokana na kushindwa kudhibiti sherehe za Kiislam pamoja na kutatua matatizo ya waislam hali inayopelekea waislam wengi kuogelea katika moto wa Jahannam.

Amesema endapo wafanyabiashara wa Kiislam Zanzibar watashirikiana na Jumuiya za Kiislam zinazoandaa sherehe za Kiislam kwa kuandaa mikakati madhubuti ya kuvidhibiti viwanja kwa kusheherekewa Eid kwa taratibu za Kiislam inaweza kupatikana nusra na kupunguza kwa kiasi kukubwa tatizo la mmomonyoko wa maadili Zanzibar.

Mhadhara huo umeandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi Elimu na Maendeleo (UKUEM) ambayo ipo mstari wa mbele katika kuandaa na sherehe za Siku kuu za Kiislam katika kumbi mbali mbali ikiwemo Kidutani na Saateni.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s