Wanawake iteteeni Hijaab – Imam Farid Hadi

Wanawake wa Kiislam Zanzibar wametakiwa kusimama imara katika kupigania vazi la Hijaab ya Mwanamke wa Kiislam.

Hayo ameyasema Imam Farid Hadi hivi karibuni katika kipindi maalum juu ya mavazi ya Kiislam kilichorushwa na Zanzibar Cable Television na Hits FM alipokuwa akijibu suala ya wanawake kulazimishwa kuvua nikab katika ofisi mbali mbali.

Amesema mbali ya mwanamke kuruhusiwa kuonekana viganja na uso lakini pia inampasa kuvaa nikab ili kuepusha fitna kwa kuficha urembo wa uzuri wa uso wake pamoja na mapambo.

“Wanazuoni wamependekeza mwanamke alokuwa uso wake ni fitna yaani mwanamke hajajipamba hajajifanya chochote yaani maumbile aliyoumbwa na Allah (S.W)ni maumbile ya kuvutia mwanamke kama huyu ni awla kustiriwa uso wenyewe ili kuondosha fitna,” alisema Imam Farid.

Katika kipindi hicho Imam Farid amewasititiza wanawake kutovaa nguo za mapambo wanapotoka nje na badala yake wajistiri kwa kuvaa mabuibui na mashingi ili kuepukana na dhambi za zinaa.

Amesema kama mayahudi na makafiri wanazingatia haki ya Mwanamke wangepiga marufuku udhalilishaji wa wanawake kama kushiriki katika mashindano ya urembo pamoja na kumtumia mwanamke katika matangazo ya biashara akiwa na mavazi yasiyostahiki.

Amefahamisha kuwa endapo mwanamke atatoka bila ya kuustiri mwili wake na kujipamba akiwa mke wa mtu wanaume ni rahisi kumtamani na kushindwa kuinamisha macho na mume hatokuwa radhi kuona mkewe anaitwa na wanaume wa nje lakini endapo mwanamke atajistiri inavyotakiwa ataheshimika na atakuwa katika himaya.

“Hizi fikra za mwanamke ajione yupo huru si katika haki hizo ni fikra za kimagharibi na kiyahudi ni za kuupiga vita Uislam ni haki gani hii? wewe mwanamke una haki ya kuheshimiwa una haki ya kuenziwa wewe lulu wa kuhifadhiwa ndani ya nyumba.”

Alisema si haki kwa jamii kumlazimisha mwanamke kutoa hijab yake na kwamba kufanya hivyo ni kukiuka maadili na kuingilia mipaka ya dini ya Kiislam na kuwataka wanawake wa Kiislam kupanga mikakati madhubuti ili kuhakikisha vazi hilo linatumika ipasavyo na kuwajengea heshima yao na ikibidi hata kuandamana katika kudao haki yao hiyo ya msingi katika dini.

Hivyo amewataka watendaji katika afisi mbali mbali za Serikali na binafsi kuheshimu Hijab ya Mwanamke wa Kiislam kwa kuweka wanawake maalum kwa kuwasachi endapo kama wana wasiwasi na wizi katika afisi zao ambapo imeonekanwa baadhi ya watu kulitumia vazi la nikab kwa kufanya uhalifu na kulitukanisha vazi hilo.

Advertisements

One Reply to “Wanawake iteteeni Hijaab – Imam Farid Hadi”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s