Wanawake wahimizwa kusoma Tawhiyd na Fiq-hi

Wanawake wa Kiislam wameshauriwa kuongeza kasi ya kusoma elimu Tawhiyd na Fiq-hi ili  iwe rahisi kwao kuendesha shughuli zao kulingana na miongozo ya dini hiyo.

Wito huo Ukhty Fatma Abdallah Mohammed wakati alipokuwa na wanawake wa Kiislam katika maonyesho ya elimu ya dini ya Kiislamu  yaliyofanyika masjid Afraa Kidongochekundu.

Amesema elimu za Tauhid na Fiq-hi pamoja na elimu nyengine za Kiislamu ni muhimu kuzifahamu mwanamke kwani bila ya kufuata miongozo inayotokana na dini watashindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Hata hivyo  Ukhty Fatma Abdallah amewapongeza wanawake wa Kiislamu kwa kuwa na mwamko mzuri wa kushughulikia masuala ya dini yao ikilinganisha na siku za hapo nyuma.

Maonyesho ya elimu ya dini ya Kiislamu kama hayo yalifanyika Al-Madrasat Hiraa ya Kisimamajongoo ambapo mgeni rasmi alikuwa Ukhty Amina Salum Khalfan ambapo aliwasisitiza wanawake kujiunga na madrasa za Qur-ani ili wajiongezee elimu zaidi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s