WAISLAM WATAKIWA KUACHANA NA SHIRKI

Waislam Zanzibar wametakiwa kujiepusha na shirki kwa kuachana na tabia ya kufuata sheria za wanaadamu zilizojengwa chini ya mfumo wa dhulma na kujali zaidi maslahi ya watunga sheria hizo.
Akizungumza katika shura ya walimu wanawake wa Madrasa za Qur-an Zanzibar huko katika ukumbi wa Al Madrasat Falaah Kijangwani Ukhty Hafsa Muhammad amesema sheria zinazotungwa wa wanaadamu hazijali maslahi ya wanaotungiwa kwa kuwa huwataka watu kuachana na sheria za Mola wao jambo linalopelekea kuwaingiza katika shirki.
“Shirki ni sababu moja ya kuenea dhulma katika ulimwengu. Hii ni kwa sababu watu wanapokosa kumuabudu na kumtii Mungu mmoja, kila mtu anakuwa na Mungu wake ambae ni shetani akiambatana na matamanio ya nafsi yake. Katika hali kama hii ambapo watu wanatii waungu wengi wa uongo badala ya Mungu mmoja wa kweli, kila mtu anavutia katika maslahi yake na kamwe hajali wengine hata kama wataangamia,” alisema ukhty Hafsa.
Amefahamisha kuwa shirki ni dhambi inayomfanya mtu kuwa katika hofu ya kudumu kwa kuwaogopa na kuwatii viumbe kama yeye ambao ni dhaifu kutokana na kumpa haki asiyestahiki.
Ukhty Hafsa amewataka waislam kujiepusha tabia hiyo kwani watakosa fursa ya kuombewa dua na waja wema na watakuwa ni watu wa motoni kutokana na kuacha kufuata mafundisho ya Qur-an na Sunna .
Aidha amesema kukosekana kwa uadilifu katika jamii ya Kiislam ni moja kati ya madhara ya ushirikina kwa kuwa kila mmoja anafuata mungu wake wa batili na kuwafanya watu waishi katika maisha mabaya duniani na kupata marejeo mabaya huko Akhera.
Amewasisitiza waislam kutubia kwa Mwenyezi Mungu na kukithirisha kufanya mambo mema kwa kufuata mafundisho ya Qur-an na Sunna pamoja na kutafuta elimu zaidi ya dini yao ili kuepukana na shirki.
Shura hiyo iliyoandaliwa na wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi, Elimu na Maendeleo chini ya Al- Madrasat Falaah hufanyika kila Jumamosi ya mwanzo wa mwezi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s