Viongozi wahimizwa Uadilifu

Viongozi wa Kiislam wanaofanya kazi katika nyanja mbalimbali wamehimizwa kusimamia uadilifu katika katika sehemu wanazofanyia kazi kwa kufuata miongozo ya Qur-an na Sunna ili kuepukana na matatizo katika jamii.

Hayo ameyasema Ukhty Mwanangano Rashid alipokuwa akizungumza na wanawake wa kiislam katika mhadhara wa kiislam uliofanyika katika ukumbi wa skuli ya Haile Sealasie mjini Zanzibar.

Amesema jamii imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbali mbali kutokana na kukosekana kwa uadilifu na badala yake jamii imekuwa mbele katika kudhulumiana hali ambayo inarudisha nyuma maendeleokatika jamii.

“Msingi mkubwa wa uongozi unapatikana kwa kufanya uadilifu kinyume chake inapatikana rushwa, unyan’ganyi na mengi mabaya yanayofanyika, kwa hali tuliyonayo sasa tunashindwa kuzuia mtu anaedhulumiwa kwa sababu tatizo ni kwamba uadilifu umekosekana tangu juu hadi chini,” alifahamisha Ukhty Mwanangano.

Amefahamisha kuwa iwapo waumini watasimamia uadilifu katika vipengele vyote kwa kuweka usawa bila ya ubaguzi ikiwa nia pamoja na ulinzi imara kwa viongozi na raia watu wataweza kuepukana na majanga mbali mbali kama mmomonyoko wa maadili na hata kudhulumiana.

Amesema ni vyema kwa watu kuachana na tamaa na mtu kutosheka na anachopata kwani kufanya hivyo kutapelekea kufanyika kwa dhulma na badala yake kufanya juhudi katika kutafuta riziki ya halali.

“Mwenyezi Mungu Mtukufu amehimiza uadilifu katika Qur-an na katika hadithi za Mtume (S.AW) ameweka mizani ili kupimia matendo ya waja wake hivyo ni vyema kila mmoja kuhakikisha kuwa anawajibika katika sehemu yake”,amesisitiza.

Mhadhara huo uliohudhuriwa na wanawake mbali mbali umeandaliwa na Jumuiya ya Umoja Wa Kiislam Uchumi, Elimu na Maendeleo (UKUEM) chini ya Al-Madrasat Falaah ya Kijangwani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s