Mahujaji wanawake watakiwa kuwa mfano bora kwa Ucha Mungu

Mwenyekiti wa jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Zanzibar (JUWAKIZA) ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tahfidhil Qur-an kwa wanawake Ukhty Zainab Thani amewataka mahujaji wanawake kuwa makini katika kutekeleza ibada ya hija ambayo ni nguzo ya tano katika uislam kwa kuwa mfano bora katika jamii.
Hayo ameyasema katika onesho maalum la ibada ya hija lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Zanzibar (JUWAKIZA) lililofanyika October 31 katika ukumbi wa shule ya maandalizi ya Kidutani mjini hapa.
Amesema lengo sahihi la ibada ya hija halipatikani bila ya mahujaji hao kuwa makini na kujipamba katika sifa ya ucha Mungu pindi watakaporejea kutoka Makka Saudi Arabia.
Amefahamisha kuwa hija ya mtu hukubaliwa kutokana na kubadilika kwa hujaji kuachana na makatazo yaliyokatazwa katika dini na badala yake kufuata maamrisho ya Qur-an na Sunna kwa ukamilifu
Onesho hilo lililokuwa la aina yake lilihudhuriwa na mahujaji wanawake wanaosafiri katika Jumuiya mbali mbali zinazoshiriki kusafirisha mahujaji ambapo mahujaji pia walipata fursa ya kuona kwa vitendo namna gain Ibada ya hija inafanywa pamoja na kufahamishwa ni vitu gani wanatakiwa kuchukua katika safari hiyo muhimu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s