Vijana Wanawake wahimizwa kupigana ‘Jihadi’ ya nafsi

Mjumbe wa Kamati ya Elimu wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi Elimu na Maendeleo (UKUEM) wanawake Ukhty Tum Ali Mussa amewataka vijana kupigana jihadi na nafsi zao kwa kuachana na mabaya ili kuweza kuleta maendeleo katika jamii.
Hayo ameyasema katika Semina kwa ya vijana wanawake waliomaliza kidato cha nne yaliyofanyika Novemba 2 katika chuo cha wanawake cha malezi ya kiislam Muslim Women Academy (MUWA) huko Chukwani.
Amesema mara nyingi nafsi imekuwa ikiamrisha mabaya na kusababisha vijana wengi kuafanya vitendo viovu hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo katika jamii na kupotea kwa maadili mema.
Amefahamisha kuwa vijana wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo katika jamii wanayoishi hivyo ni vyema wakaitumia fursa hiyo katika njia zinazomridhisha Mwenyezi Mungu kwa kuacha makatazo ya dini yao na kufuata maamrisho na kwamba kila mmoja ataulizwa jinsi gani ameutumia ujana wake.
Aidha amehimiza juu kutunza wakati kwa kufanya mambo ya kheri kwa kujua kuwa kila wanalofanya ni ibada pamoja na kutafuta njia za halali za kutafuta riziki na kujipamba na sifa njema ili kuwa kigezo bora katika jamii wanayoishi.
“Kila mmoja ajitengeneze mwenyewe kiroho, aubebe na kuutetea Uislam kwa nguvu zote. Kushirikiana pamoja katika harakati za kuiokoa jamii kwani hii si kazi ya walimu wa Madrasa na Masheikh, hii ni kazi ya waislam wote,” alifahamisha Ukhty Tum.
Akifungua semina hiyo Mwenyekiti wa jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Zanzibar (JUWAKIZA) ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tahfidhil Qur-an kwa wanawake Ukhty Zainab Thani amewataka wana semina kuifanyia kazi elimu wanayoipata kwa kufuata maamrisho yaliyowekwa na Mwenyezi Mungu.
“Elimu ni miongoni mwa ibada iliyo tukufu, na jambo likiwa faradhi huwa ni tukufu mbele ya Allah, kwani huwezi kufanya ibada yoyote bila ya kuisomea! Mwenyezi Mungu hapokei ibada isiyo na elimu….”
“Mkazo mkubwa uliotiliwa katika elimu haikugaiwa kuwa hii ni ya dunia nah ii ya akhera tumejuulishwa tu umuhimu wake kuwa ni ibada tukufu, na kuwa haina mwisho na kunayanyuliwa darja wenye elimu. Lilo muhimu ni kusoma kwa ajili ya Allah,” alisisitiza Ukhty Zainab Thani.
Nae mwalimu wa Chuo hicho Ustadha Ramla Abdulramhan amewataka Waislam kujitokeza kwa wingi katika kuwapa vijana muongozo sahihi wa maisha kwa mujibu wa mafundisho ya Qur-an na Sunna.
Amesema lengo la semina hiyo kwa vijana ni kuweka msingi bora wa maisha katika jamii ili iweze kuondokana na tatizo la mmomonyoko wa maadili ambapo amesema pia ni funzo kwa taasisi mbali mbali za Kiislam katika kupigana kuiokoa jamii.
Semina hiyo ya siku tano imedhaminiwa na Uongozi wa Muslim Women Academy (MUWA) imewashirikisha vijana wanawake 50 kutoka unguja na pemba na inatarajiwa kufungwa Novemba 7.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s