“Vijana zidisheni mapenzi kwa Mola wenu” UKUEM

Vijana wametakiwa kuzidisha mapenzi kwa mola wao kwa kufuata maamrisho ya dini yao na kuacha makatazo.
Hayo ameyasema Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi Elimu na Maendeleo Wanawake Ukhty Fatma Salim Saleh alipokuwa akifunga semina ya siku tano ya mafunzo ya Kiislam kwa wanafunzi wanawake waliomaliza kidatu cha nne huko katika Chuo cha Wanawake cha Malezi ya Kiislam Muslim Women Academy (MUWA) yaliyofanyika Novemba 7 Chukwani.
Amesema muumini wa dini ya kiislam hana hiari ya kujichagulia ya kufanya anayotaka kwa kuachana na misingi ya Qur-an na Sunna kwani kufanya hivyo kutapelekea kuharibikiwa katika maisha yake.
“Isiwe ni kujichagulia tu hili unalipenda ukalifata na hili silipendi hata kama ni amri ni kitu wajibu kwako ukaliacha. Naamini mtakuwa mbele katika kusimamisha sala na kujistiri,” alisema.
Amewataka wanasema kuwa macho na kutahadhari juu ya kuingia katika maovu kwa kuyajua mema na mabaya kwani sheitani hatoacha kumchezea binaadamu kwa kumpeleka katika njia ya upotofu.
Amesema Mwenyezi Mungu mlezi wa viumbe wote hapendi kumtia mtu motoni ila walifanya mabaya na kumuasi hivyo ni vyema kuyatumia mafunzo hayo kwa kufuata maamrisho ya dini na kuacha makatazo.
Amefahamisha kuwa waislam hawana budi kujihami kwa Mwenyezi Mungu kwa kujitahidi kuutumia muda wao vizuri pamoja na kujiendeleza katika masomo ya fani mbali mbali na kuweza kupata mafanikio hapo baadae.
Aidha ametoa wito kwa waislam kuacha kushughulikia masomo ya kidunia pekee na badala yeke wawe mbele katika kuhakikisdha kuwa wanagangaika kwa kuisoma Qur-an na kuifahamu.
“Watu wamemaliza mitihani ‘O’ level na ‘A’ level wamo katika kusubiri matokeo na kujiendeleza katika field nyengine. Wengine English course, wengine Computer course, wengine ushoni na wengine ufundi ili hayo yaje yawafae baadae! Husikii mtu kuhangaika akasema anatafuta mwalimu amsomeshe Qur-an au mirathi katika Uislam. Ni vitu muhimu lakini watu wanaona ya kale na wanataka ya usasa,” alifahamisha Ukhty Fatma.
Katika risala ya kumaliza mafunzo hayo wanafunzi wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo hayo kivitendo ambapo waliweza kujifunza elimu ya Tawheed, Akhlaq, Mapishi, kazi za mikono pamoja na Afya na mazoezi ya viungo na kusema mafunzo hayo yatawawezesha kujiajiri wenyewe.
Katika semina hiyo chuo cha wanawake cha malezi ya Kiislam Muslim Women Academy (MUWA) imewatunukia shahada wanafunzi 50 kutoka Unguja na Pemba.

Advertisements

One Reply to ““Vijana zidisheni mapenzi kwa Mola wenu” UKUEM”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s