Wanawake wa Kiislam watakiwa kuutumia afya zao kwa ajili ya Allah

Waislam wametakiwa kuzitumia vizuri afya zao wakiwa wazima kwa kukithirisha kufanya ibada kabla hayajawafikia mauti au maradhi.
Wito huo umetolewa na Ukhty Mwanaate Juma alipokuwa akiwasilisha mada juu ya Jichumie mambo matano kabla ya matano katika Shura ya walimu wanawake wa madrasa za Qur-an iliyofanyika Novemba 7 huko katika ukumbi wa Al Madrasat Falaah Kijangwani.
Amesema Binaadamu hawezi kuutumia vizuri muda wake kwa kumuabudu Mola wake katika wakati wa maradhi hivyo ni vyema kujiandaa sasa kwa kukithirisha ibada ili asijute akiwa mgonjwa.
“Unaweza ukawa mgonjwa huwezi hata kunywa tone la maji mwenyewe, huwezi hata kujiondosha ulipo mpaka ubebwe… hapo utajutia afya yako ambayo hukuitumia vizuri ipasavyo, ipasavyo jichumie kwa afya yako, mema kwa ajili ya Akhera yak oleo, afya ni taji juu ya kichwa cha mwenye afya halioni isipokuwa mgonjwa,” alifahamisha Ukhty Mwanaate.
Amewahimiza Waislam kuwa wakarimu, kuacha ubahili, kufanya mema kama walivyofanyiwa na Mwenyezi Mungu na kutoa misaada kwa mafakiri, masikini, na kutozuia haki yao hiyo ikawa ni sababu ya Mwenyezi Mungu kumzuilia mtu katika kupata riziki zake.
“Nini unajua kuhusu dini yako na Mtume wako? Kwa fadhila zako, ewe Muislam wakati ni rasilimali yako kwa hivyo usiupoteze katika mambo ya kipuuzi na michezo, jua kuwa utaulizwa kuhusu hayo,” alisisitiza.
Shura hiyo imeandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Kiislam, Uchumi, Elimu na Maendeleo (UKUEM) wanawake chini ya Al- Madrasat Falaah ya Kijangwani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s