Waislam watakiwa kuachana na vyombo vya habari vinavyochochea zinaa.

Waislam wametakiwa kujiepusha na vyombo vya habari vinavyochangia kuenea kwa zinaa.
Hayo yamesemwa katika Ukhty Ramla Abdulrahman alipokuwa akitoa mada juu ya zinaa na madhara yake katika shura ya walimu wanawake wa madrasa za Qur-an iliyofanyika Disemba 5 katika ukumbi wa Al Madrasat Falaah Kijangwani.
Amesema muislam ni lazima aishi maisha ambayo Allah ameyaridhia kwa kujiepusha na vishawishi mbali mbali vinavyochangia kumuingiza mtu katika zinaa kama kusikiliza nyimbo au kutazama tamthilia pamoja na kusoma magazeti yenye vishawishi vya kimapenzi.
“Tunaishi katika dunia ambayo watu wakiwemo baadhi ya waislam, huyavalia njuga na kuyatangaza maovu pasi na kimeme pamoja na kuyakataza mema hadharani bila ya hofu. Hali hii itatufikisha mahali ambapo yale mabaya takaonekana kuwa ndio mema na yale mema yakaonekana kuwa mabaya,” alifahamisha Ukhty Ramla.
Amesema sera na akhlaki za kimagharibi zimekuwa zikiushambulia Uislam na waislam wakaelekea katika kuzisheherekea mila hizo kwa kila shubitri na kupelekea kutokemea mabaya pindi wanapoyaona yanatendeka hadharani.
Amefahamisha kuwa kuyafumbia macho mabaya ya zinaa katika jamii ndiko kulikopelekea madhara makubwa katika uhai wa viumbe ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa watoto wa zinaa pamoja na maradhi mbali mbali ya zinaa ikiwemo gonjwa hatari la Ukimwi na kwamba.
“Matokeo yake basi kwa hapa duniani na kwa yale yunayoyaona na kutafakari ni madhara makubwa mno kuenea kwa maradhi ya uasharati ikiwemo Ukimwi na kutapakazana kwa kusema hayana dawa, wataalamu wamo mbioni kutafuta dawa, hakuna dawa ila kuacha zinaa basi hatimae maradhi haya yatahama endfapo jamii haitakuwa na walevi, wazinifu…” alisema Ukhy Ramla.
Aidha amewasisitiza waislam kuachana na yote yanayosababisha kufanyika kwa zinaa kwa kufuata kikamilifu mafundisho ya Qur-an na Sunna kwa kutochanganyika ovyo na wanaume bila kuvaa hijabu ya kisheria kutopeana mikono wanawake na wanaume wanaoweza kuoana kitendo ambacho ni haramu katika uislam.
Shura hiyo imeandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi Elimu na Maendeleo (UKUEM) chini ya Al Madrasat Falaah ya Kijangwani imehudhuriwa na walimu wanawake mbali mbali wa Madrasa za Unguja.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s