WANASIASA WAACHE MZAHA NA QUR’AN-BARAZA LA WANAWAKE WA KIISLAM

Msimamizi Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Kiislamu Tanzania Sheikh Abdalla Abass Mnubi ameiomba ofisi ya Mufti Zanzibar kupiga marufuku kusomwa Qur’an katika mikutano ya kampeni za vyama vya siasa kwani kufanya hivyo ni kukishushia hadhi kitabu hicho kitukufu.

Akizungumza na waislamu mara baada ya shura ya baraza hilo iliyofanyika hivi karibuni huko Dole Sheikh Mnubi amesema ni kinyume na maamrisho ya dini Qur’an kusomwa mahali ambapo hapana utulivu na nidhamu ya kidini.

Aidha amewataka maimamu kuzungumzia utukufu wa Qur’an na umuhimu wa kukitukuza na kukifuata kitabu hicho ili jamii iweze kufanikiwa katika mambo yao.

“Utaona Qur’an inasomwa baada ya msomaji kumaliza kusoma tu pale inawekwa nyimbo, hii inapelekea kuidhalilisha Qur’an na hatujui Mwenyezi Mungu atatupa adhabu ipi!”

“Tutakaa tunasema maisha magumu pengine ndio adhabu yenyewe hiyo mwenyezi Mungu anatulipa, ndio adhabu yenyewe hiyo” alisema Sheikh Mnubi.

Amewataka waislam kuwa tayari kutetea Qur’an na kuilinda kwa hali na mali kama nchi mbali mbali za Waislam wanavyoandamana kupinga kuchomwa kwa kitabu kitukufu cha Qur’an.

“Wanasiasa wameifanya Qur’an haiendani na Uislam na wamefanya kama utamaduni, zamani walikuwa wakiambiwa wanachanganya dini na siasa, ni haki yetu waislam kupinga dini na siasa!” alisema.

Amelisema Qur’an inakataza mambo mbali mbali amabyo wanasiasa wanayafanya kama kupiga ngoma, kucheza ngoma, kuchanganyika wanawake na wanaume pamoja na wanawake kutembea utupu.

Amefahamisha kuwa waislam hawatakiwi kuichezea dini yao na wanatakiwa kuwa madhubuti na makini na kuchukia pale yanapoharibiwa matukufu ya dini yao na kuwataka waislam kutubia na kuachana na tabia hizo chafu.

Amsisitiza haja kwa wanasiasa kuisoma vyema dini ya Kiislam ili kuachana na yale yote yanayomchukiza Mwenyezi Mungu pamoja na kutubia kwa kurudi kwake ili waweze kufanikiwa katika mambo yao.

Wakati huo huo wananchi wa Dole wamezitaka Jumuiya za Kiislam, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa afisi ya Mufti kuzuia ujengwaji ovyo wa makanisa katika kijiji chao ili kuondokana na maudhi wanayofanyiwa na waumini wa dini ya kikristo.

Wakizungumza katika shura kilichofanyika hivi karibuni huko Dole wamesema ujengwaji wa makanisa hayo kunapelekea kwa watoto wa kiislamu kuingia katika makanisa jambo ambalo linawarudisha nyuma waislam.

Wamesema kukithiri kwa makanisa katika kijiji chao kumepelekea baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo kuwarai watoto kwa kudai kuwasomesha masomo ya ziada bure na na kinyume chake kuwafundisha mambo ya dini hiyo kwa njia ya siri.

“Yaani linatukera hasa suala hili la ujengwaji wakamanisa, linatuharibia watoto wetu kwani washaanza kuigiza ibada zao” alisema Bi Zainab Khamis.

Aidha wamelalamikia hali ya watoto wao kutohudhuria katika madrasa kutokana na viongozi hao wa makanisa kuutumia muda huo kwa kuwasomesha katika makanisa jambo ambalo linawaletea usumbufu mkubwa.

Hata hivyo baadhi ya waislam walisema mara nyingi katika kipindi cha kampeni za siasa waumini wa dini ya kikristo huutumia muda huo kwa kuimarisha Makanisa na dini yao hali ambayo inawaumiza sana waislam.

Wamesema hali inatokana na watu wengi kushughulikia siasa na mara tu unapomalizika uchaguzi watu hushtukia kuna makanisa katika sehemu wanazoishi.

Advertisements

One Reply to “WANASIASA WAACHE MZAHA NA QUR’AN-BARAZA LA WANAWAKE WA KIISLAM”

 1. Assallam aleykum,
  Kusema kweli hilo ni tatizo sugu sana na limeanza kwa muda mrefu na linaendelea kuhusu kusoma quraan wakati wa mikutano ya kisiasa. Kwani katika mkusanyiko ule kunakuwa hakuna utulivu , hasa akinamama wengi wao mavazi yao sio mazuri na wengine vichwa wazi jee hiyo quraan inafika? au tanataka laana kwa Mwenyezi Mungu, yale masharti ya usomaji quraan hayafatwi kabisa. Nakuombeni waislam tushikamane kulizungumzia suala hilo kwa nguvu zetu zote.

  Suala la pili kuhusu makanisa na watoto wakiislam kwenda makanisani ni suala nyeti zaidi. Nafikiria kuwa waislam tuko nyuma sana kwani hilo ni suala la si la kulalamika kwa serikali itusaidie. Ni vyema tujiulize sisi kama waislam wa Dole tumefanya nini?

  Ni vyema, na sisi waislam tukaanzisha mafunzo yetu ya ziada katika madrasa zetu na kutafuta walimu wazuri wa kutusaidia ili vijana wetu wahudhurie katika mafunzo ya ziada.

  Inahitaji waislamu wenzangu tujipange vizuri ili kuwanusuru watoto wetu wasije kufuata dini za kikafiri kwani wenzetu hawalali wanafikiria njia mbali mbali za kuwaingiza watoto wetu katika dini yao.

  Hivi sasa mimi nimeshuhudia wakati wa krismasi wakristo wa Jumbi wameendesha misa katika Skuli ya Haile Selesie basi watoto wa kiislamu wakike na wakiume na wasichana wari walikuwa wakishiriki katika misa zile jee unafikiria baada ya mwaka moja vijana wangapi wameshafuata ukiristo na imani ya kiislamu imepotea kwenye mioyo yao.

  Lazima waaisilamu tuuungane na tuache tofauti zetu ili kuunusuru uislamu ,waislamu na kitabu kitakatifu cha Allah.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s