WANAWAKE WA KIISLAM WATAKIWA KUSOMA KWA BIDII

Wanawake wa Kiislam Zanzibar wametakiwa kuamka kwa kusoma kwa bidii na kuwasomesha watoto wao elimu ya dini ya Kiislam pamoja na kuwahifadhisha Qur-an ili waweze kuondokana na matatizo mbali mbali katika maisha yao.

Wito huo umetolewa na mwalimu mkuu wa chuo cha malezi ya wanawake wa Kiislam cha Nairobi Ukhty Azra Abdulmajid Khuwaja katika mahafali ya pili ya chuo cha malezi ya wanawake wa Kiislam Zanzibar Muslim Women Academy (MUWA) huko Chukwani.

Amesema ili kurudisha haiba na mbegu ya Uislam Zanzibar ni lazima waislam kurudi kwa kuisoma kuisoma dini yao na kuifanyia kazi katika sekta mbali mbali na kuachana na tabia ya kusoma elimu ya dunia pekee.

“Tumeacha dini yetu, tumeacha elimu yetu na tunashughulikia mambo mengine! Tuna kazi kubwa sana kama hatujarudisha elimu ya dini tutakumbwa na balaa,” alisema Ukhty Azra.

Amefahamisha kuwa elimu ya akhera inampa mtu utukufu pamoja, utulivu, inamuwezesha kufanya ibada kama za hijja, sala, saumu, zaka na nyenginezo kwa uhakika hivyo ni vyema kwa waislam kusoma kwa bidii ili waweze kujadiliana na watu katika dini yao.

Wakitoa maoni yao juu ya suala la uvaaji wa vazi la hijab ya mwanamke wa Kiislam ambalo wanawake wengi wananyanyaswa kwa kutopatiwa kazi katika ofisi mbalimbali walezi wamewataka wanawake hao kutoregeza misimamo yao na badala yake waendelee kutii amri ya Mwenyezi Mungu.

Wamemewahimiza wanawake kuacha kutii amri za viumbe kwani kufanya hivyo kutapelekea kuingia katika adhabu za Mwenyezi Mungu na badala yake mawe mstari wa mbele katika kuelimisha jamii ili ilielewe vazi hilo.

Katika risara yao wahitimu wa chuo cha Muslim Women Academy (MUWA) wameahidi kuifanyia kazi elimu waliyoipata pamoja na kuomba kupatiwa vitabu pamoja na kukamilishwa kwa ujenzi wa dakhalia na walimu wa somo la computer katika chuo hicho pamoja na kuwataka walimu kuzidisha juhudi ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.

Chuo hicho kinatoa elimu ya Dini ya Kiislam pamoja na lugha, elimu ya amali kama ushonaji, ufumaji na mapishi.

Jumla ya wanafunzi 26 wametunukiwa shahada ambapo mwanafunzi Farhat Khamis aliibuka kuwa mwanafunzi bora katika masomo na mwanafunzi bora katika nidham ni Saada Ali ambapo walipewa zawadi.

Advertisements

2 Replies to “WANAWAKE WA KIISLAM WATAKIWA KUSOMA KWA BIDII”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s