Waislam someni elimu ya ndoa – Abdulrahman Bakar Muhana

Wanawake wa kiislamu nchini wametakiwa kuipa kipaumbele zaidi elimu ya ndoa ili kuepusha kuvunjika kwa ndoa zao.

Wito huo umetolewa na Ustadh Abdulrahman Bakari Muhana kutoka taasisi ya Islamic  Foundation na mwendeshaji wa kipindi cha Familia kinachorushwa kila siku  saa tano usiku na Iman FM alipokuwa akizungumza na kinamama wa kiislamu katika kongamano la kuhamasisha akina mama hao huko katika Al-Madrasat Baswairi  iliyopo Daraja Bovu Mivinjeni  Mjini Unguja.

Amesema ndoa nyingi za kiislamu huvunjika kutokana na ukosefu wa elimu hivyo waislamu hawana budi kusimama imara katika kutafuta elimu ili kunusuru ndoa zao.

Amefahamisha kuwa elimu ni ufunguo wa maisha hivyo waislam wafahamu kuwa ili maisha ya ndoa yawe bora yanahitaji elimu ya kutosha ambayo itawajengea heshima na kuepuka mifarakano isiyokuwa ya lazima.

Akichangia mada Bi Asha Ali  Makame amesema kuvunjika kwa ndoa  kiuzembe kunatokana na ukosefu wa elimu imani, subira, ukosefu wa kizazi pamoja na kutelekezwa kwa mwanamke na waume zao.

Hata hivyo amesema lengo la kongamanohiloni kuwahamasisha waumini wa kiislamu hasa akina mama kupatiwa elimu ya ndoa ili kuziwezesha ndoa zao zisivunjike na kutokuwepo kwa migogoro na kupatikana kizazi chenye malezi bora.

Wakati huo huo Ustadh Abdulrahman Bakar Muhanna amewataka wazazi na walezi kuwafundisha watoto wao malezi bora katika misingi ya Kiislamu ili kuwa na tabia njemakama alivyofundisha Mtume Muhammad S.A.W.

Hayo ameyasema katika mhadhara uliofanyika Madrasat Baswaair, juu ya malezi ya watoto.

Amesema jamii imeharibika kutokana na kuiga utamaduni wa nje ambapo wazazi na walezi ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa hali ambayo italeta  hasara kwao na taifa.

Amesema ni vyema wazazi kuwaamrisha watoto wao maadili mema kamayalivyo mafundisho ya Mtume Muhammad S.A.W.

Nae Mkuu wa Taaluma wa Madrasat Baswaair  Maalim Juma Mohd amesema madrasa hiyo imeamua kufanya muhadhara huo ili kuizindua jamii ya Kiislamu kufuata mambo mema.

Mkuu huyo amewataka waislamu nchini kuelekeza michangoyaokatika vyuo vya madrasa na katika misikiti mbalimbali ili kuendeleza uislamu.

Advertisements

6 Replies to “Waislam someni elimu ya ndoa – Abdulrahman Bakar Muhana”

  1. ASALAAM ALAYKUM NI MAWAIDHA MAZURI SANA UST. LAKINI NA WANAUME NAO WAPATE MAFUNZO KWANI MAFUNZO MENGI WANAOPEWA NI WANAWAKE NA KUONEKANA KAMA WANAUME WAO WANAJUA, KUMBE HAWAJUI WAJIBU WAO NA WAO NDIO WANAOANZA KUYUMBISHA NDOA. MIMI NIMEACHWA KWA SABABU HUYO MUME KUTOJUA WAJIBU WAKE KWANGU.

    1. waalikum salaamu warahmatullah wbarakatuh!!,
      kwelmnalosema ni kwel ila kikubwa ni watu kuelimishana wao kwa wao mfano umeona mwenzio hakufanyi hivyo inavyokustahili mwelekeze ama mume au mke, mwambie fanya hivi na usinifanyie hivi. kuwa mpole mwonyeshe nn afanye, mengi ya kusema ila hayo yanatosha

  2. Asalam aleykum ni kweli tunaweza kuelimishana lkn bora elim imfikie muhusika kwani atakavyo ipokea kwako tofauti akiipokea kwa huyo muhusika huwezi jua chanzo cha migogoro,baadhi ya wanaume wanaona makosa yapo kwa wake zao tu wao hawana makosa na wachache watakaokubali kukosolewa na wake zao na kuyakubali makosa yao muhimu kila muhusika akapate elimu.

  3. Asalam alaikum w.w., Elimu wapewe wanandoa wote wawili kabla hawajakutanishwa. wazaza wa pande z0te mbili wajihusishe na elimu ya ndoa ya wanao.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s