Waislam watakiwa kuifanyia kazi Qur’an

Waislam nchini wametakiwa kuisoma Qur’an na kuifanyia kazi ili iweze kuwasaidia katika maishayaoya kila siku.

Akizungumza na wanawake wa madrasa za Bweleo Wilaya ya Magharibi Ukhty Amina Salim Khalfan alisema alisema mtu hawezi kuijua Qur’an bila ya kuyajua mazingira.

Alifahamisha kuwa mtu mwenye kuisoma na kuifanyia kazi Qur’an hupata fadhila nyingi kuliko mwenye kuisoma na kuihifadhi bila ya kuifanyia kazi.

“Mwenyezi Mungu ataenda kuwalipa wenye kuisoma Qur’an na kuifanyika kazi”

Alisema Ukhty Amina.

Hata hivyo amewataka Waislam kuwasomesha watoto wao elimu ya dini na dunia waweze kuwa wasomi wa baadae na kuweza kuwasaidia katika maishayaoduniani na Akhera.

Alisema baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya kuwasomesha watoto wao elimu ya dini pekee au ya dunia pekee hali ambayo inapelekea kupatikana kwa vijana wasio na upeo mzuri wa elimu.

Hivyo amewataka waislam kubadilika na kuwasomesha watoto wao kwa ajili ya akhera na duniani.

Aidha ukhty Amina amewataka waislam kushiriki katika marekebisho ya katiba ili waweze kupata haki zao za msingi.

Alisema wakati umefika kwa waislam kuacha kukaa kimya na badala yake wajitokeze kudai katiba yenye kutetea maslahi ya diniyaoili katiba hiyo iweze kuwasaidia wao na kizazi chao cha baadae.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s