Wazazi watakiwa kuwafuatilia watoto wao

WAZAZI wametakiwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao katika vyuo na kwengineko na kuachana na tabia ya kuwaachia walimu pekee ili kurahisisha mafunzo ya watoto wao.

Akizungumza katika mahafali ya Muslim Women Acvademy Chukwani. Ukhty Rukia Matttar amesema wana jukumu la kufuatilia maendeleo ya watoto wao kwani wana wajibu wa kujua maendeleoyaona shida wanazokutana nazo katika masomoyao.

Alisema ni vyema wazazi kukutana na walimu kwa kutoa ushauri na rai mbali mbali juu ya maendeleo ya elimu kwa watoto waokamaalivyokuwa akifanya Mtume Muhammad (S.A.W) kwa Masahaba wake.

Alisema mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho ikiwemo lugha ya kiarabu ni jambo kubwasanana la kujivunia na kuwataka wanafunzi hao kuyafanyia kazi masomo hayo na kuielimisha jamii ili isiwe hasara kwao.

“Siku hizi kuna vikundi mbali mbali vya kidunia vinaundwa, wakati umefika na sisi tutumie taaluma tuliyopata hapa kuanzisha Jumuiya ambazo zitaendeleza na kukuza kile tulichokipata hapa,” alisema Bi Rukia.

Amewataka kutumia bidhaa wanazozalisha chuoni hapo kwa kuanzisha vikundi ambapo itakuwa rahisi katika kupata soko na kujiendeleza zaidi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s