KUHUSU SISI


Asalam Aleykum!
Asalam Aleykum!

KWA JINA LA ALLAH MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU.

Kila sifa njema ni zake  Allah (Subhaanahu wa Ta’ala)  na rehema na amani zimshukie Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  na jamaa zake na Sahaba zake na waja wema katika Uislam.

Karibu katika Weblog ya MWANAMKE WA KIISLAM ambayo ni Weblog  ya Kiislam inayojihusisha na kutoa elimu juu ya mambo mbali mbali ya Wanawake wa Kiislam wanayotakiwa kufanya katika Uislam pamoja na kutoa mafunzo ya adabu za katika maisha ya waislam.

Lengo halisi ni kuendeleza na kuifanyia kazi kauli yake Allah SUBHANA HU WA TAALA isemayo: 

“Nyinyi ndio Umma bora kuliko Umma zote zilizodhihirishwa kwa watu (Ulimwenguni) mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamuamini Allah.” (Aal- Imran 110)

Aidha zaidi ni kubadilisha sura ya maisha ya mwanamke wa kiislam na kwa kuwafahamisha mambo mbali mbali wanayoyajua na wasiyoyajua kupitia Qur-an na Sunnah.

P3130002

Pamoja na hayo MWANAMKE WA KIISLAM  itakuwa inakujuulisha harakati mbali mbali zinazoendeshwa na Wanawake wa Kiislam wa Zanzibar katika Jumuiya zao ili kuweza kuihamasisha jamii kuamka katika Dini yao ya Kiislam.

Ili kuendeleza harakati za Kiislam na kupeleka mbele Dini ya Allah Mtukufu MWANAMKE WA KIISLAM pia inakaribisha maoni mbali mbali kutoka kwa wasomaji pamoja na kuyafanyia kazi.

Karibu sana!

 

 

Kwa maelezo zaidi au kutuma Makala mbali mbali za Kiislam tuma kwa anuani ifuatayo:

islamicwomen@ymail.com

Advertisements

6 Replies to “KUHUSU SISI”

 1. kwakweri ndogu waisilam tunamuasi sana Mwenyezi Mungu hasa wanawake tumezidi sana kumuasi Mwenyezi Mungu utakuta ndani ya nyumba mama wa Kiisilam tabia zake sizuri je? watoto wake watakuwaje ikiwa mama kila siku akiwa nasheda basa anaenda kwa waganga je? Mungu hayupo ama tunataka kupoteza umma wa Mtume (SAW.

 2. ningependa kujua kitabu cha bi rabwa abdalla cha mapishi nani kakupeni authority muweke kenye mapishi.ni serious sana.kinaitwa mapish ya mwambao mimi ni mwanawe wa kumzaa

  1. ASALAAM ALEYKUM!
   NASIKITIKA KWAMBA MAPISHI HAYA HAYANA UHUSIANO NA KITABU CHOCHOTE HILI JINA LIMETOLEWA TU NA HICHO KITABU CHA MAMA YAKO HATUKIJUI HATA KUKIONA HATUJAKIONA.
   AHSANTE.

 3. Asalamun alaikum… nimefurahi kujua hii blog ibayo inafunza mambo mengi.. Allah awabarik walioiunda Ameen. nakupendeni nyote kwa ajili ya Allah. Fii amani lah.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s