RIYADHUSSALIHIYN


MAUA YALIYOCHUMWA KUTOKA KATIKA MABUSTANI YA WATU WEMA (RIYADHU SSALIHIN)

 • MILANGO MAALUM KWA WANAWAKE.

 

Bustani ya Maua
Bustani ya Maua

 

 

 

 

Mlango nambari 173: Uharamu wa mwanamke kusafiri peke yake.

590. Abdullah bin Abbas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesimulia kuwa alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: Asikae faragha katu mwanamme na mwanamke ela awe pamoja nae (mwanamke) maharimu, wala asisafiri ela pamoja na maharimu wake.” Mtu mmoja akauliza: “Ewe mtume wa Allah, mke wangu ametoka kwenda kuhiji, nami nimeandikwa katika vita kadha wa kadha?” Akamwambia: “Nenda ukahiji pamoja na mkeo.” Muttafaq.

591. Abu Huraira (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Si halali kwa mwanamke anaemwamini Allah na siku ya mwisho asafiri mwendo wa mchana na usiku ela awe pamoja na maharimu wake.” Muttafaq.

Mlango nambari 279:Uharamu wa kumtazama mwanamke ajnabi na kumtazama kijana mwenye uso mzuri pasipo na dharura ya ki-sharia.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Waambie waumini wanaume wainamishe macho yao …” [24:30]. Allah amesema: “Hakika masikio, na macho, na moyo, hivyo vyote vitaulizwa.” [17:36]. Allah amesema: “(Allah) Anajua khiyana ya macho na yanayoficha vifua.” [40:19]. “Allah amesema: “Hakika Mola wako yuko katika malindizo.” [89:14]

943. Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nilimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu mtu kutazama kwa ghafla (bila ya kukusudia) akaniambia: “Geuza macho yako.” Muslim.

944. Abu Said (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwanamme asitazame utupi wa mwanamme, wala mwanamke asitazame utupu wa mwanamke, wala mwanamme asilale na mwanamme mwenziwe katika nguo moja, wala mwanamke asilale na mwanamke mwenzie katika nguo moja.” Muslim.

Mlango nambari 280:Uharamu wa kukaa faragha na Ajnabi

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu “Na mnapowauliza haja wakeze, waulizeni nyuma ya pazia.” [33:53]

945. ‘Uqba bin Amir (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Tahadharini na kuingia kwa wanawake!” Mtu mmoja katika Ansari akauliza: “Nieleze akiwa ni shemeji?” Akamwambia shemeji ni mauti!” Muttafaq.

Mlango nambari 281:Uharamu wa wanaume kujifananisha na wanawake na wanawake kujifananisha na wanaume katika mavazi, miondoko n.k.

946. ‘Abdullah bin Abbas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake na wanawake wanaojifananisha na wanaume.”

Katika riwaya nyengine imesema: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wanaojishabihisha na wanawake na wanawake wanaojishabihisha na wanaume.” Bukhari.

947. Abu Huraira (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Aina mbili za watu wa motoni sijawaonapo (hawapo katika zama zangu), watu walio na mijeledi mfano wa mikia ya ng’ombe wanawapiga watu kwa mijeledi hiyo (kwa dhulma), na wanawake waqliovaa nguo na bado wako utupu wakitembea kwa maringo huku wakiyanyonga mabega yao na wakiwafunza wengineo kutenda kama hivyo, vichwa vyao ni kama nundu za ngamia-bukhti wanaochechemea. Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake, na kwa hakika yake husikika umbali kadha wa kadha.” Muslim.

Ngamia-bukhti: Aina ya ngamia wenye shingo ndefu. 

Mpendwa Msomaji Mwanamke wa Kiislam inakaribisha maoni na maelezo juu ya Kipengele au mlango wowote unaopenda kuuzungumzia.

Karibu sana!

Advertisements

14 Replies to “RIYADHUSSALIHIYN”

 1. MASHALLAH MASHALLAH MASHALLAH, MOLA AKUZIDISHIENI KULIKO HAYA MEMA MNAYOTUFAIDISHA NAYO. NIMEFAIDIKA SANA NA NZURI SANA SANA SANA. JAZAKUMULLAH KHAIRAN WAJANNATU NAEEM INSHAALLAH.

 2. Mashallah , Mabruk .
  Nina Swali,
  Nini hukumu ya mwanamke kuchonga nyusi au kunyoa kabisa.
  Inaruhusiwa katika sheria za dini yetu tukufu ?

  1. Asalaam aleykum,
   Ahsante kwa kutembelea Blog ya Mwanamke wa Kiislam.

   Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
   Kunyoa nyusi au kuzichonga ni haramu, sawa ikiwa ni kwa kujipodoa kwa ajili ya mume, au kwa kujipamba mwanamke binafsi.
   Allah Anasema “Alilokuleteni Mtume lichukueni, na alilowakatazeni liacheni” (Al-Hashr: 7)
   Na katika jumla ya mambo aliyotukataza Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni kunyoa nyusi.
   عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال ((لعن الله الواشمات والمستوشمات والنامصات والمتنمصات والمتفلجات للحسن المغيرات خلق الله ((البخاري و مسلم
   Kutoka kwa ‘Abdullahi bin Mas’uud (Radhiya Allahu ‘anhu) kwamba: ((Allah Amewalaani watu wenye kuwachanja wenzao (tattoo) na wenye kuchanjwa, na wenye kuwanyoa wenzao nyusi na wenye kunyolewa na wenye kuchonga meno yao (kama kufanya mwanya) kwa ajili ya kujipamba kubadilisha maumbile ya Allah) [Al-Bukhaariy Hadiyth Namba 5948 na Muslim Namba 2125]
   Ama nini cha kufanya, baada ya kuwa mlikuwa ni katika wafanyao hivyo? Jukumu lenu ni kurejea kwa Allah kwa kufanya toba ya kweli, sambamba na kuwalingania dada zenu wengine waachane na mwenendo huo, kwa lugha nzuri na mawaidha mema.
   Jambo hili la kumuasi Allah na Mtume Wake (Swalla-LLahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakika halikutiliwa mkazo na dada zetu kabisa. Na mara nyingi linapokemewa kwa dada zetu wao hawalioni kama ni jambo la maana kukatazwa, wengine hulazimishwa japokuwa wao hawataki na waume zao kama ilivyo hali ya muulizaji wa kwanza. Ama wengine husema “Lakini si najipamba kwa ajili ya mume wangu” au “Mume wangu anapenda nitoe nyusi” au “Itakuwaje nyusi zinijae nisizitoe?” na mengi husemwa ambayo yanadhihirisha kutotilia mkazo jambo hili ovu la kuasi amri. Amesema Mtume (Swalla-LLaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam):
   ))لا طاعة لمخلوق في معصية الخالق)) رواه أحمد وهو صحيح
   ((Hakuna kumtii kiumbe katika maasiya ya Muumba)) [Ahmad ikiwa sahiyh]
   Vile vile:
   قال صلى الله عليه وسلم: ((على المرء المسلم السمع والطاعة فيما أحب وكره إلا أن يؤمر بمعصية، فإن أمر بمعصية فلا سمع ولا طاعة)) رواه مسلم .
   Kasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam) ((Muislamu inampasa asikie na atii katika anayoyapenda na anayoyachukia isipokuwa anapoamrishwa katika maasiya. Anapoamrishwa kufanya maasiya basi asisikie wa kutii)) [Muslim]
   وقال: (( لا طاعة في معصية الله إنما الطاعة في المعروف)) رواه مسلم
   Na kasema (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa Sallam): ((Hakuna kutii katika kumuasi Allaah, ama kutii ni katika mema)) [Muslim]
   Tuchukue mfano mwema aliotuonyesha pia Abu Bakr wakati wa ukhalifa wake:
   وقال أبو بكر رضي الله عنه حين بويع بالخلافة: “أطيعوني ما أطعت الله فيكم، فإن عصيته فلا طاعة لي عليكم”
   “Nitiini nitakapomtii Allah kwenu, na nitakapomuasi basi msinitii”
   Muislamu inampasa atambue kuwa kumtii kiumbe katika maasiya ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) haitomsaidia kitu akhera kwani huko yatakuja ni majuto tu na adhabu na pia hata kiumbe unachomtii inampasa na yeye amche Allah na akhofu adhabu siku ya Qiyaamah kwani ajue kuwa kumuamrisha mwenziwe katika maasi au kutomkataza basi yeye atamuombea apewe adhabu mara mbili na juu ya hivyo atamuombea laana kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
   ((يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا)) ((وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا)) ((رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا ))
   ((Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungelimtii Allah na tungelimtii Mtume!)) ((Na watasema: Mola wetu! Hakika sisi tuliwatii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio waliotupoteza njia)) ((Mola wetu! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa)) [Al-Ahzaab: 66-68]
   Hivyo hakuna mmoja atakayemfaa mwenzake katika kuamrishana au kuridhishana katika maasi.
   Pia ndugu zetu wa kike wajihadhari sana na baadhi ya wanaojiita Mashekhe wanapoulizwa kama ilivyo katika hali ya muulizaji wa tatu, akamjibu kwanza inafaa, kisha mara ya pili akakanusha. Bila shaka huyo hakuwa na elimu ya kutosha kuweza kutambua katazo lililokuja katika Hadiythi hiyo ya kulaaniwa mwanamke mwenye kunyoa nyusi.
   Anapotaka Muislamu kuuuliza Swali la dini hasa linalohusu mambo ya haram na halali na yenye hatari kama hii, ni bora kumtafuta Shaykh mwenye elimu hasa ya dini ili asije kupata Fatwa itakayompotoza badala ya kumuongoza, na kisha bila ya kujua naye Muislamu akawapa wenzake Fatwa hiyo kama alivyofanya bila ya kujua muulizaji wa Swala la tatu.
   Inampasa muulizaji wa Swali la tatu naye arudie kuwakanya aliowapa Fatwa hiyo isiyo sahihi na awafahamishe vilivyo, naye arudi kwa Mola wake na kuomba Maghfirah.

   Tuwe na tahadhari na baadhi ya mashekhe kwani kuna wanaohalalisha hilo kwa sababu itikadi yao potofu inaruhusu mwanamke kunyofoa nyusi kwa ajili ya mumewe! Wajiulize hao wanaoambiwa hivyo na hao wenye itikadi hizo, ikiwa atanyofoa au kunyoa nyusi kwa mumewe, je, pindi akitoka nje atazuiaje wale wasio maharimu zake kuwaona bila nyusi zao na hali wenye itikadi hizo hawavai Niqaab? Hata ikiwa wataamua kuvaa Niqaab, maadam ni jambo limeshaharamishwa, hivyo haliwezi kuhalalika kwa vijisababu kama hivyo vya kumrembea mume au kuvaa Niqaab ukitoka n.k.
   Natumai nimekujibu Ahsante sana na endelea kufaidiaka na Mwanamke wa Kiislam.

   1. Assalam aleikum, naombeni kuuliza katika hilo la mwanamke kua na kichwa km nundu ya ngamia, inakuaje hapo? Niliwahi kuuliza mahali nikajibiwa ni ile mwanamke kuweka banio la nywele nyuma ya kichwa chake, vipi kuhusu wale wanawake wenye nywele ndefu, wakiziweka tu vizuri bila kubana na mabanio ya nywele yale makubwa pia haifai?

 3. mashallah ni blog nzuri sana hii ndo faida ya mitandao kuusiana mambo ya kheri nasikufundishana maasi Allah akulipe kwa haya akuzidishie ilmu amiin

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s